Login for faster access to the best deals. Click here if you don't have an account.

CONSTRUCTION NI NINI

Jan 14th, 2023 at 10:27   Beauty & Health   Arusha   23 views

-- TSh

  • construction-ni-nini-big-0
  • construction-ni-nini-big-1
Location: Arusha
Price: -- TSh

Constipation Ni Nini?

Constipation ni ugumu wa kutoa uchafu wote kwenye tumbo, hii ni kutokana na choo kuwa kigumu. 

 

Kwa maaana nyingine ni kwamba ni hali ya kupungua kwa kasi ya utoaji kwa uchafu/kinyesi tumboni ama kupata choo kigumu na kukosa choo kwa muda mrefu.

 

Nini Husababisha Constipation/ Kukosa Choo Au Kupata Choo Kigumu?

Umewahi kujiuliza kwanini unakosa choo kwa muda mrefu au kupata choo kigumu na kwa shida, huku ukipata maumivu makali wakati wa kujisaidia?

 

 

 Kwa kiasi kikubwa kukosa choo na choo kigumu husababishwa na mkusanyiko wa sababu.

 

Sababu hizi ni pamoja na

 lishe yako, kiasi gani mwili wako unaushugulisha, na na jinsi unavocontrol stress/msongo wa mawazo.

 

 Sababu kubwa kabisa ikiwa ni ulaji wa vyakula vyenye kiwango kidogo sana cha kambakamba/fibers na matumizi kidogo ya maji .

 

Unapopata constipation baadhi ya dalili huanza kujitokeza kwenye mfumo wa chakula kama; 

 

kupungua wa kasi ya utoaji wa kinyesi au uwepo wa kiasi kidogo cha kinyesi, kuchelewa kwa utolewaji wa kinyesi kuliko kawaida. 

 

Kama unaumwa magonjwa kama Irritable bowel syndrome (IBS) au ugonjwa mwingine kwenye mfumo wa chakula basi yaweza kuwa ndio chanzo cha constipation.

 

Sababu za kukosa choo na choo kigumu

Hapa chini ni sababu zinopelekea upate constipation

Lishe mbovu: Vyakula vilivyosindikwa sana, sukari, nafaka iliyokobolewa, pombe.

 Vyakula vilivyoongezwa sukari na kemikali za kutunza chakula kisiharibike na mafuta mabaya huleta ugumu kwenye utengenezaji na utolewaji wa kinyesi na hivo kukupelekea kukosa choo kwa muda mrefu.

 

 

Msongo wa mawazo: Watu wanaopata msongo mkubwa wa mawazo huharibu mpangilio wa homone zao pamoja na kuathiri uzalishaji wa visambaza taarifa kwenye mwili na hivo kusababisha shida kwenye misuli, kupata mcharuko/mpambano ndani ya mwili (inflammation) na kuathiri ufanyaji kazi wa enyzmes ambazo husaidia kumeng’enya chakula.

 

 

Kutoshughulisha mwili: Mazoezi yanasaidia kuimarisha mzunguko wa damu kwenye mfumo wa chakula na kuimarisha misuli na hivo kurahisisha utolewaji wa kinyesi. Utafiti unasema watu wanaotumia mda mwingi wakiwa wamekaa hasa maofsini wanaongoza kwa kuapata matatizo ya kukosa choo kwa mda mrefu.

 

 

Matumizi ya baadhi ya vidonge: Baadhi ya vidonge husababisha kukosa choo kwa muda mrefu na kupata choo kigumu. Mfano dawa za kupunguza maumivu, dawa za kuconrtol stress, dawa za kulevya, virutubisho vya calcium na magnesium na antiacids.

 

 

Ukuaji wa bacteria wabaya kwenye mfumo wa chakula: Bacteria wazuri/normal flora waliopo kwenye mfumo wa chakula tunawaita probiotics husaidia kwenye uchakataji wa chakula. Ndio maana kuna umuhimu wa kula vyakula vyenye kambakamba kwa sababu ni mbolea nzuri kwa bacteria wazuri kukua na kufanya kazi.

 

 

Matatizo ya tezi ya thyroid na matatizo mengine ya homoni: Matatizo kama kisukari, kukoma hedhi, maumivu kabla ya hedhi na ufanyaji kazi hafifu wa tezi ya Thyroid huweza kusababisha kupata constipation. 

 

Magonjwa mengine ni kama Pakinson disease, ajali ya uti wa mgongo na matatizo mengine ya neva yanaweza kusababisha Constipation.

 

 

Upungufu wa magnesium: magnesium husaidia ufanyaji kazi mzuri wa misuli na hivo kusaidia utolewahi mzuri wa kinyesi.

 

 

 Baadhi ya tabia hatarishi wakati umeenda chooni: tabia hizi ni kama kujisaidia kwa haraka na ukaaji mbaya unapokuwa chooni hasa watumiaji vyoo vya kukaa huchangia kuongeza ukubwa wa tatizo na kisha kupelekea kupata ugonjwa wa bawasili

Umri mkubwa na kukosa usingizi huchangia pia kukosa choo kwa muda mrefu

Wasiliana nasi kwa maelekezo zaidi na tiba