Login for faster access to the best deals. Click here if you don't have an account.

JUA UGONJWA WA GOUT DALILI,MADHARA,VISABABISHI,TIBA

Jan 30th, 2022 at 22:50   Beauty & Health   Arusha   49 views

-- TSh

  • jua-ugonjwa-wa-gout-dalilimadharavisababishitiba-big-0
  • jua-ugonjwa-wa-gout-dalilimadharavisababishitiba-big-1
Location: Arusha
Price: -- TSh

kawaida, gauti inaweza kutokea ghafla(acute) au ikawa sugu(chronic). Kwa ile inayotokea ghafla huwa na maumivu makali na mara nyingi huathiri kiungo kimoja tu wakati gauti sugu inaweza kuathiri kiungo zaidi ya kimoja na huambatana na hali ya kujirudia ya maumivu na uvimbe kwenye viungo. Visababishi vyake Gauti husababishwa na kuwepo kwa kiwango kikubwa kuliko kawaida cha tindikali ya uriki katika damu. Hali hii hutokea iwapo mwili wa mgonjwa unatengeneza uriki nyingi kuliko kawaida au unashindwa kutoa tindikal ya uriki mwilini kama inavyotakiwa. Ongezeko hili husababisha mrundikano wa tindikali ya uriki katika majimaji yanayozunguka viungo yanayoitwa synovial na hatimaye kutengeneza vijiwe vidogovidogo vya tindikali ya uriki ambavyo husababisha viungo kuvimba na hatimaye kuathirika. Vihatarishi -Wanaume huathiriwa zaidi kuliko wanawake ingawa wanawake waliokoma kupata hedhi huathiriwa zaidi. -Aidha, unywaji pombe unachangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa ugonjwa huu pamoja na matumizi ya baadhi ya dawa kama vile za kutoa maji mwilini ambazo kwa ujumla husababisha ongezeko la kiwango cha uriki katika damu. Vihatarishi vingine ni pamoja na kuwa na -ugonjwa wa kisukari -magonjwa ya figo, unene uliokithiri -upungufu wa damu unasababishwa na seli mundu (sickle cell) au aina nyingine za upungufu wa damu, pamoja na saratani ya damu (leukemia). Dalili za ugonjwa huo Dalili kwa kawaida huhusisha kiungo kimoja au vichache. Viungo vinavyoathiriwa zaidi ni pamoja na kidole kikubwa cha mguuni, magoti, au kiwiko cha mguu. -Wagonjwa huwa na maumivu yanayoanza kwa ghafla, hususan nyakati za usiku. Mara nyingi mgonjwa hudai anasikia maumivu makali kama kitu kinachokata, kupwita au mifupa inayosagana. -Viunganio katika mwili hubadilika na kuwa na joto, kuvimba na kuwa na nyekundu (hujionyesha zaidi kwa watu wenye ngozi nyeupe). Kwa kawaida mgonjwa hulalamika maumivu makali ikiwa ataguswa kwenye kiungo chenye matatizo. -Shambulio linaweza kudumu kwa siku kadhaa kabla mgonjwa hajapata nafuu, pia laweza kujirudia mara kwa mara. -Pia mgonjwa anaweza kujihisi homa. Baadhi ya wagonjwa hupata gauti sugu ambayo huwaletea madhara sugu katika viungo (chronic arthritis) hali ambayo husababisha mgonjwa kujihisi maumivu na muda mwingi kushindwa vizuri kutumia viungo vyake. -Wagonjwa wa muda mrefu huwa pia na vinundu chini ya ngozi inayozunguka viungo vilivyoathirika. Vinundu hivi ni ishara ya muhimu kwa madaktari. Vipimo -Kiwango cha tindikali ya uriki katika damu. Hata hivyo, si kila aliye na kiwango kikubwa cha tindikali ya uriki katika damu huwa na gauti. -Kiwango cha tindikali ya uriki katika mkojo -Uchunguzi wa maji maji yanayozunguka viungo (synovial fluid) kuchunguza vijiwe katika viungo. -X ray ya kiungo kilichoathirika. -Uchunguzi wa utando unaozunguka joint) Matibabu Matibabu hujumuisha matumizi ya dawa, lishe pamoja na mabadiliko katika tabia na mienendo ya kimaisha ya mgonjwa. Dawa hutumika mara tu mgonjwa anapopata shambulio la ghafla. Dawa hizo ni pamoja na: Lishe na mabadiliko katika mfumo wa maisha husaidia pia kuthibiti na kumwepusha mgonjwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya gauti. Karibu kwa ushauri na suluisho juu ya ugonjwa huu Ushauri: -Tuache pombe -Tupunguze ulaji wa vyakula vyenye viasili vya purine (aina ya protini) kama vile nyama ya mbuzi, maini au figo #ugonjwawagaout #dalilizagauti #madharayagauti #Guti