Login for faster access to the best deals. Click here if you don't have an account.

KUJUA TOFAUTI YA UCHAFU WA KAWAIDA NA USIO WAKAWAIDA NA TIBA YAKE

Jan 30th, 2022 at 07:14   Beauty & Health   Arusha   108 views

-- TSh

  • kujua-tofauti-ya-uchafu-wa-kawaida-na-usio-wakawaida-na-tiba-yake-big-0
Location: Arusha
Price: -- TSh

TOFAUTI KATI YA UCHAFU WA KAWAIDA NA USIO WA KAWAIDA UTOKAO UKENI Baadhi ya uchafu utokao ukeni huwa ni ishara ya kuonyesha afya ya uke wako. Je, unafahamu tofauti iliyopo kati ya uchafu wa kawaida na usio wa kawaida utokao ukeni?  Kutokwa na uchafu ukeni ni sehemu ya asili ya kuwa mwanamke, lakini wakati mwingine mabadiriko ndani yake yanaweza kuonyesha tatizo fulani. Sasa hebu tuangalie aina tofauti za uchafu unaotoka ukeni ili kwamba uweze kujua kwamba ni muda gani uchafu wako unakuwa sio wa kawaida.   Uchafu Wa Asili Unaotoka Ukeni Kazi kubwa ya uke wako ni kutoa uchafu unaokuwa kwenye mfuko wa uzazi pamoja na viungo vyote vya mfumo wa uzazi. Asidi ya asili inayokuwa kwenye uke wako hufanya kazi ya kuzuia maambukizi na husababishwa bakteria wazuri wa asili wanaokuwa ukeni mwako. NUKUU: Katika siku ya kawaida uke wako hujisafisha wenyewe kwa kutoa uteute msafi mweupe wenye utelezi. Uwiano wa asili wa uke unaweza kuharibiwa na kitu chochote kinachoingizwa ndani ukeni.   Uchafu Wa Kawaida   Kwanza, yafaa vyema kuelewa kwamba wanawake wote hutokwa na uchafu ukeni. Tezi ndani ya uke wako au mlango wa kizazi hutoa kiwango kidogo cha uteute ambao hutiririka nje ya mwili wako kila siku, huku ukiwa umebeba seli zilizozeeka. Uchafu wa kawaida ukeni mwako husaidia kusafisha uke, pamoja na kuufanya uwe laini na usiwe na maambukizi wala vimelea wengine. Uke unakuwa hauna harufu mbaya hata kidogo. Uchafu wa kawaida ukeni mara nyingi huonekana msafi au kama maziwa vile pale unapokauka juu ya chupi yako au nguo ya ndani. Mara nyingi unaweza kuona uchafu ambao ni mzito wenye kuvutika kama kamba kamba vile. Unaweza ukauita mweupe msafi na wenye kuteleza kama kamasi vile.   Mambo ambayo yanaweza kutoa uwiano sawa wa asidi ya asili ukeni na kupelekea kuwapo kwa maambukizi, ni pamoja na;   Kutia vitu vibaya ukeni kama vile asali, pipi kifua, maji ya limao, nkKuoshea maji ya ukokoKuoshea vitu vyenye marashi makali ukeniUjauizitoKisukari1.     Kipindi Cha Hedhi Huathiri Uchafu Utokao Ukeni   Mzunguko wako wa hedhi una kazi kubwa katika aina ya uchafu unaotoka ukeni unauona katika mzunguko wa mwezi mzima. Takribani ya nusu kati ya vipindi vya hedhi, utaona muongezeko wa uchafu wa kawaida ambao unakuwa mweupe kama ute wa yai la kuku. Hali hii huongeza unyevunyevu na uchafu unaoashiria yai kupevuka. Huu ni wakati wa siku za hatari na unaweza ukapata ujauzito. Je, unafahamu kwamba unaweza kupatwa maambukizi kwa urahisi sana kabla au wakati wa ujauzito? Hii ni kwasababu ya uwiano wa kawaida wa asidi ya asili ukeni kutofautiana wakati wa mzunguko wako wa hedhi, na kusababisha kiwango cha asidi kushuka chini siku chache kabla na wakati wa hedhi.   1.     Dalili Za Uchafu Usio Wa Kawaida   Ni muhimu sana kutambua ishara za uchafu usio wa kawaida utokao ukeni kwasababu inaweza kuwa ishara ya maambukizi au magonjwa mengine katika mwili wako. Unapoona hali ya kutokwa na uchafu ukeni ambao unatoka na kuongezeka ghafla, basi hii inaweza kuwa ni ishara ya tatizo. Badiriko jingine ambalo linaweza kuashiria tatizo ni uchafu ambao ni wenye rangi ya njano yenye kung’aa au wenye rangi ya ukijani. NUKUU: Uchafu mzito wa mabonge bonge au kila uchafu wa majimaji unaweza pia kuashiria kwamba kuna kitu kinakosekana ukeni mwako. Baadhi ya dalili zinazoweza kuashiria maambukizi ni pamoja na; Mabadiriko katika rangi, mnato kama maziwa ya mgandoMuwasho, au kutojisikia vizuri sehemu za ukeUke kuwa na hali ya kuwaka moto wakati wa kukojoaKutokwa na damu hata kama sio kipindi cha hedhiHarufu kali ikiambatana na uchafu wenye rangi ya njano, ukijani, au kijivu mweupe.Kama unatokwa na uchafu ukeni pamoja na ishara nilizozitaja hapo awali, basi unapaswa ufike hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi na matibabu. Je, Ni Aina Gani Tofauti Za Uchafu Zinazoashiria? ·        Ikiwa kama uchafu wako ni mweupe na mzito na wenye mabonge na una muwasho ukeni au hali ya kuwaka moto, basi hii inaashiria kabisa kuwa una maambukizi ya fangasi sehemu za siri ·        Kama una uchafu ambao ni mwingi kuliko kawaida, ambao ni wenye majimaji na wenye rangi ya  kijivu na wenye harufu mbaya kama shombo la samaki, hii inaashiria kuwa una bakteria ukeni. ·        Kama unatokwa na uchafu ukeni ambao huongezeka ghafla katika kiwango, ambao ni wa kijani au njano ambao una harufu mbaya, au unasababisha dalili za ukeni, basi unapaswa kufika hospitali na kumuona daktari ili kuweza kupima na kujua chanzo ili kupata matibabu.   1.     Maambukizi Ya Kawaida Ukeni   Visababishi vya kawaida vya uchafu usio wa kawaida ukeni ni pamoja na;  ·        Malengelenge(Trichomoniasis)  ·        Pangusa(Chlamydia) ·        Kisonono(Gonorrhea) ·        Kusahau kuondoa ped ukeni   ·        Maambukizi mengine ya zinaa  ·        Fangasi sehemu za siri  ·        Bakteria ukeni