Login for faster access to the best deals. Click here if you don't have an account.

MISUNDO SUNDO,VISABABISHI,DALILI,MADHARA NA TIBA YAKE

Jan 4th, 2022 at 14:33   Beauty & Health   Arusha   368 views

-- TSh

  • misundo-sundovisababishidalilimadhara-na-tiba-yake-big-0
  • misundo-sundovisababishidalilimadhara-na-tiba-yake-big-1
  • misundo-sundovisababishidalilimadhara-na-tiba-yake-big-2
  • misundo-sundovisababishidalilimadhara-na-tiba-yake-big-3
Location: Arusha
Price: -- TSh

HAMU TIBA YA UGONJWA WA KUOTA VINYAMA/MASUNDOSUNDO/VIGWARU SEHEMU ZA SIRI(GENITAL WARTS) FAHAMU TATIZO LA KUOTA VINYAMA/MASUNDOSUNDO/VIGWARU SEHEMU ZA SIRI (GENITAL WARTS) Asalaam Alaykum warhmatullah wabarakatul,Ni matumaini yetu unaendelea vyema mpendwa msomaji wa blog hii karibu darasani kwa mara nyingine tena leo tunazungumzia tatizo la kuota vinyama,chanzo chake na namna ya kutibu tatizo hili Ugonjwa wa kuota Vinyama sehemu za siri/Masundosundo/vigwaru au Genital warts ni tatizo la kuota vinyama laini vidogo vinavyoota kwenye ngozi au utando laini unaozunguka maeneo ya siri. Vinaweza kutokea kwenye uume, uke, mrija wa mkojo [urethra], vulva, shingo ya kizazi [cervix], au maeneo ya kuzunguka njia ya haja kubwa au ndani yake. Huu ni ugonjwa unaoenezwa kwa njia ya kujamiiana [sexually transmitted infection (STI)]. VISABABISHI VYA UGONJWA WA KUOTA VINYAMA/MASUNDOSUNDO/VIGWARU SEHEMU ZA SIRI {GENITAL WARTS} Ugonjwa wa masundosundo husababishwa na jamii ya virusi wanaoitwa Human papilloma virus (HPV). Kuna zaidi ya aina 70 tofauti za virusi wa HPV ingawa si wote wanaosababisha masundosundo kwenye maeneo ya siri [genital warts]. Baadhi ya aina nyingine za HPV husababisha masundosundo kwenye ngozi inayozunguka sehemu nyngine za mwili kama vile kwenye mikono au miguu. Tafiti kadhaa zimeonesha kuwa baadhi ya aina za virusi wa HPV pia husababisha saratani ya shingo ya kizazi [carcinoma of the cervix] kwa wanawake au saratani ya njia ya haja kubwa [anal cancer] kwa jinsia zote mbili. Aina hii ya virusi hujulikana pia kama high-risk HPV. Pamoja na kwamba ugonjwa wa masundosundo kwenye maeneo ya siri umejitokeza kwa kasi kubwa hasa baada ya kuwepo kwa janga la UKIMWI, watu wengi waliopatwa na ugonjwa huu huwa hawaoneshi dalili zozote zile. Kwa mfano, kwa wanawake, virusi wa HPV wana uwezo wa kusambaa mpaka maeneo ya ndani kabisa ya kuta za uke au shingo ya kizazi [cervix] bila kuonekana wala kuhisiwa kwa urahisi. Kama tulivyotangulia kueleza hapo awali, maambukizi ya HPV husambaa kutoka kwa mtu mmoja mpaka mwingine kwa njia ya kujamiiana kunakohusisha njia ya haja kubwa, uke au ngono ya mdomoni. Mara baada ya kuambukizwa, huweza kuchukua mpaka muda wa wiki sita hadi miezi 6 kwa masundosundo kuwa dhahiri, ingawa baadhi ya wagonjwa wanaweza kukaa hata miaka kadhaa bila kuwa na dalili yeyote ile. Aidha imeonekana pia kuwa si kila mtu anayejamiina na aliye na maambukizi ya HPV au mwenye masundosundo anaweza naye kupata ugonjwa huu. MAKUNDI YALIYO KATIKA HATARI YA KUPATA UGONJWA WA KUOTA VINYAMA/VIGWARU/MASUNDOSUNDO SEHEMU ZA SIRI{GENITAL WARTS} Watu walio katika makundi haya wapo katika hatari kubwa zaidi ya kupatwa na masundosundo kwenye maeneo ya siri • Wenye wapenzi wengi • Kufanya ngono isiyo salama/ ngono zembe • Kuanza vitendo vya ngono katika umri mdogo • Watumiaji wakubwa wa sigara pamoja na pombe • Kupatwa na maambukizi ya virusi wa herpes na wakati huo huo kuwa na msongo mkali wa mawazo • wajawazito • kuwa na upungufu katika mfumo wa kinga mwilini kwa sababu ya magonjwa mbalimbali au kwa sababu ya matumizi ya dawa fulani fulani kwa watoto wadogo, ukiona mtoto amepata masundosundo basi ni vema kufanya uchunguzi ikiwa amewahi kubakwa au kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji. DALILI ZA KUOTA VINYAMA/VIGWARU/MASUNDOSUNDO SEHEMU ZA SIRI[GENITAL WARTS} Masundosundo [genital warts] huonekana kama vioteo laini vinavyojitokeza juu ya ngozi ingawa wakati mwingine vinaweza kuwa vidogo mno kiasi cha kutoweza kuonekana vizuri kwa macho ya kawaida. Kwa wanaume, vioteo hivi hutokea zaidi kwenye uume, ngozi ya pumbu, eneo la mitoki, mapajani pamoja na maeneo ya kuzunguka nje ya njia ya haja kubwa au ndani yake; wakati kwa wanawake hutokea ndani ya uke au njia ya haja kubwa, nje ya uke au ngozi ya nje kuzunguka njia ya haja kubwa, au ndani ya uke kuzunguka eneo la shingo ya kizazi. Kwa wale wanaopenda kufanya ngono ya mdomoni [oral sex], wanaweza kupatwa na masundosundo/genital warts kwenye maeneo ya kuzunguka mdomo, lips, kwenye ulimi na hata kwenye utando unaozunguka koo. Dalili nyingine ni kama vile mgonjwa kujihisi kukosekana kwa hisia [kufa ganzi] maeneo yaliyozungukwa na masundosundo, kwa wanawake kuongezeka kwa utoko/ uchafu sehemu za siri, kuwashwa sana maeneo ya siri na wakati mwingine kutokwa na damu ukeni mara baada ya tendo la ngono. Hata hivyo dalili hizi hutokea mara chache sana. Wanawake wengi vijana wanaojihusisha na vitendo vya ngono [sexually active] huambukizwa sana ugonjwa huu lakini wengi wao hupona bila hata kuhitaji matibabu, wakati wanaume wanaoambukizwa, wengi wao huwa hawaoneshi dalili zozote za ugonjwa ingawa wanaweza kuwaambukiza wenzi wao bila ya wao kujua. UCHUNGUZI NA VIPIMO Kwa wanawake, uchunguzi wa ugonjwa wa masundosundo/genital warts hujumuisha uchunguzi wa maeneo ya nyonga [pelvic examination] ambapo daktari huchunguza eneo hilo kwa kutumia vifaa maalum vinavyomuwezesha kuona uwepo wa masundosundo na wapi vilipo. Wakati fulani, kunyunyizia dawa yenye tindikali ya acetic acidhusaidia kufanya masundosundo kuonekana kwa urahisi zaidi. Wakati mwingine daktari anaweza pia kufanya kipimo cha pap smearkwa ajili ya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi [kwa vile kama tulivyoona hapo awali, zipo aina fulani fulani za HPV ambazo husababisha saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake]. Kwa wanaume, uchunguzi wa maeneo ya siri ni muhimu sana ili kufahamu kama kuna masundosundo au la.