SABABU ZA MIPASUKO KWENYE ULIMI NA TIBA
Jan 7th, 2023 at 10:44 Beauty & Health Dar es Salaam 54 viewsTATIZO LA MIPASUKO KATIKA ULIMI
Ulimi wa mtu kwa kawaida hautakiwi kuwa na mipasuko ya aina yoyote . Sasa hawa watu wenye ulimi uliopasuka huwa hawana maumivu , isipokua tu labda kama kuna chakula kimekwama kwenye hiyo mipasuko ndio muhusika atahisi maumivu
Mipasuko hii huweza kuwa iliyochimbika sana au kiasi tu. Wazee ndio hupatwa sana na hii mipasuko ya ulimi , japo yeyote yule anaweza kuwa na ulimi wa hivi. Wanaume ndio huwa zaidi na tatizo hili kuliko wanawake
NINI HUSABABISHA HALI HII ?
Hadi sasa , wataalamu hawajui ni nini hupelekea hali hii ya mipasuko kwenye ulimi , japo ina amini kwamba watu wenye undugu (genetics) huweza kuwa na tatizo hili na wengine wasiwe nalo . mfano katika familia , unaweza kuta mzazi ana tatizo hili na watoto pia . Mfano : Kuna tafiti ilifanyika na ikabaini kwamba watu wa South Africa ni 0.6% tu ya watu wote ndio wana tatizo hili la mipasuko kwenye ulimi , lakini Katika Taifa la Israel 30.6% ya watu wote ndio wana hii hali. Sasa unaweza ona kwamba swala la jamii fulani yenye mfanano wa kigenetiki huweza kuwa na hii hali ya mipasuko na jamii nyingine isiwe nayo
TATIZO HILI LA MIPASUKO KATIKA ULIMI HUWA NA UHUSIANO NA MAMBO KAMA HAYA :
Geographic tongue
Kuvimba kwa lips na uso kutokana na matatizo ya neva .
Upungufu wa virutubisho muhimu kwa mwili n.k japo hii huwa na mchango mdogo
MATIBABU Tatizo hili kiufupi , lina hitaji tiba , isitoshe kisababishi hakijulikani , .
USHAURI
Ubaya wa hii mipasuko ni kwamba endapo chakula kitabakia kwenye hiyo mipasuko , itapelekea bacteria kuzaliana , maumivu na hata kupelekea harufu mbaya ya kinywa na hata kuchangia meno kuharibika Muhusika pia anakua katika mazingira marahisi ya kushambuliwa na fungus wa kinywa (candinda ablicans) , ikiwa imekutokea basi dawa zipo , onana na daktari sasa nikupe suruhisho la kudumu.
Hakikisha unafanya usafi wa kinywa angalau mara mbili kila siku , na uwe na utaratibu wa kumuona daktari wa meno angalau mara mbili kwa mwaka karibu nikusaidie