Login for faster access to the best deals. Click here if you don't have an account.

SABABU ZINAZO FANYA UKOSE CHOO NA MADHARA YA KUKOSA CHOO

Jan 5th, 2023 at 09:18   Beauty & Health   Arusha   43 views

1 TSh

  • sababu-zinazo-fanya-ukose-choo-na-madhara-ya-kukosa-choo-big-0
  • sababu-zinazo-fanya-ukose-choo-na-madhara-ya-kukosa-choo-big-1
  • sababu-zinazo-fanya-ukose-choo-na-madhara-ya-kukosa-choo-big-2
  • sababu-zinazo-fanya-ukose-choo-na-madhara-ya-kukosa-choo-big-3
Location: Arusha
Price: 1 TSh

Sababu za kukosa choo na choo kigumu

Hapa chini ni sababu zinopelekea upate constipation

1.Lishe mbovu:

2.Vyakula vilivyosindikwa sana,

3.matumizi makubwa ya sukari, nafaka iliyokobolewa, pombe. Vyakula vilivyoongezwa sukari na kemikali za kutunza chakula kisiharibike na mafuta mabaya huleta ugumu kwenye utengenezaji na utolewaji wa kinyesi na hivo kukupelekea kukosa choo kwa muda mrefu.

4.Msongo wa mawazo: Watu wanaopata msongo mkubwa wa mawazo huharibu mpangilio wa homone zao pamoja na kuathiri uzalishaji wa visambaza taarifa kwenye mwili na hivo kusababisha shida kwenye misuli,

5.kupata mcharuko/mpambano ndani ya mwili (inflammation) na kuathiri ufanyaji kazi wa enyzmes ambazo husaidia kumeng’enya chakula.

6.Kutoshughulisha mwili: Mazoezi yanasaidia kuimarisha mzunguko wa damu kwenye mfumo wa chakula na kuimarisha misuli na hivo kurahisisha utolewaji wa kinyesi.

Utafiti unasema watu wanaotumia mda mwingi wakiwa wamekaa hasa maofsini wanaongoza kwa kuapata matatizo ya kukosa choo kwa mda mrefu.

7.Matumizi ya baadhi ya vidonge: Baadhi ya vidonge husababisha kukosa choo kwa muda mrefu na kupata choo kigumu.

Mfano dawa za kupunguza maumivu, dawa za kuconrtol stress, dawa za kulevya, virutubisho vya calcium na magnesium na antiacids.

8.Ukuaji wa bacteria wabaya kwenye mfumo wa chakula:

Bacteria wazuri/normal flora waliopo kwenye mfumo wa chakula tunawaita probiotics husaidia kwenye uchakataji wa chakula.Ndio maana kuna umuhimu wa kula vyakula vyenye kambakamba kwa sababu ni mbolea nzuri kwa bacteria wazuri kukua na kufanya kazi.

Matatizo ya tezi ya thyroid na matatizo mengine ya homoni: Matatizo kama kisukari, kukoma hedhi, maumivu kabla ya hedhi na ufanyaji kazi hafifu wa tezi ya Thyroid huweza kusababisha kupata constipation.

Magonjwa mengine ni kama Pakinson disease, ajali ya uti wa mgongo na matatizo mengine ya neva yanaweza kusababisha Constipation.