Login for faster access to the best deals. Click here if you don't have an account.

UGONJWA WA P.I.D(PELVIS INFLAMATORY DESEASE)

Nov 30th, 2022 at 20:50   Beauty & Health   Dar es salaam   67 views

-- TSh

  • ugonjwa-wa-pidpelvis-inflamatory-desease-big-0
Location: Dar es salaam
Price: -- TSh

UJUE UGONJWA WA P.I.D

Maambukizi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke kwa kitaalamu Pelvic Inflamatory Diseases au kwa kifupi PID, ni moja ya matatizo ambayo huwaathiri sana wanawake.

Kwa kawaida maambukizi haya huusisha shingo ya uzazi (cervix) hali ambayo hujulikana kama cervicitis, nyama ya mfuko wa uzazi (endometrium) ambayo kitaalamu huitwa endometritis, na mirija ya uzazi (fallopian tubes) hali ijulikanayo kitabibu kama salpingitis.

PID husababishwa na nini?_

Pamoja na aina kadhaa za vimelea kuhusishwa na PID, vimelea vya jamii ya Neisseria Gonorrhoeae pamoja na Chlamydia trachomatis ndivyo vinavyoongoza kwa umaarufu zaidi katika kusababisha PID kwa akina mama.

Je mwanamke huambukizwaje PID?

Kuna njia kadhaa ambazo mwanamke anaweza kuambukizwa PID.

Njia hizo ni pamoja na

Kufanya ngono isiyo salama. Maambukizi ya njia ya uzazi hasa kipindi mara baada ya kujifungua (au postpartum period)

Maambukizi ya njia ya uzazi mara baada ya kutoa mimba kwa njia zisizo salama (post abortion) au mara baada ya mimba kutoka (miscarriage)

Kutumia vipandikizi vya ndani ya mfuko wa uzazi (IUCD) kama njia mojawapo ya uzazi wa mpango. Kuambukizwa kupitia damu iliyo na vimelea vya PID.

Dalili za PID ni zipi?

Zipo dalili kadhaa za ugonjwa huu wa PID.

Miongoni mwa dalili hizi ni :- Mwanamke kuhisi maumivu ya tumbo hasa maeneo ya chini ya kitovu

Kupata maumivu ya mgongo.

Mwanamke kupata utoko mchafu sehemu za siri.

Utoko huu huambatana na harufu mbaya. Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa.

Kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Kutoka damu bila mpangilio wakati wa hedhi.

Kupata homa.

Wakati fulani kuhisi kichefuchefu na Pia kutapika.

Ugonjwa huu wa Pelvic Inflammatory Diseases P.I.D unakuwa kwa Kasi kubwa na baadhi ya wanawake hupata madhara makubwa baadae hususa